Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji 3,000 waokolewa Mediterenia-IOM

Wahamiaji 3,000 waokolewa Mediterenia-IOM

[caption id="attachment_318626" align="aligncenter" width="615"]iomwahamiaji

Karibu wahamiaji 3,000 wameokolewa siku moja wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterenia wakitokea Kaskazini mwa Afrika kuelekea barani Ulaya, limema shirika la kimataifa la wahamiaji IOM.

Kwa mujibu wa IOM, meli kadhaa zilihusishwa katika uokozi wa makundi kadhaa ya watu siku ya Alhamisi, ambapo wengi wa waliookolewa walipelekwa nchini Italia huku wahamiaji wengine zaidi ya 500 wakirejeshwa nchini Libya.

Manusura hawajafahamika, lakini IOM inasema kwamba mabaki ya maiti sita wamepatakina katika siku za hivi karibuni katika Pwani ya Libya.

Shirika hilo limeeleza kuwa idaidi ya watu wanaotumia bahari ya Mediterenia sasa ni kutoka sehemu kadhaa ikiwamo kutoka Kuwait kama anavyoeleza msemaji wake Joe Millman.

( Sauti Millman)

‘‘Kwahiyo tunabaini hili na inashangaza kiwango kwa ambacho Uturuki inandelea kuwa njia, kwa mfano mgogoro wa Iraq au Syria, hapo yaweza kueleweka lakini kinachoshangaza ni idadi ya nchi ambazo hupitia Uturuki ili kufika Ugiriki , na kwamba tuashuhudia wahaiti, wadominican kutoka visiwa vya Caribbean wakija Ugiriki kutoka Uturuki.Ni idadi ndogo lakini inaongezeka.’’