Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno la wiki: Chakari au mwanamajiri

Neno la wiki: Chakari au mwanamajiri

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno Chakari au mwanamajiri. Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA

Bwana Zuberi anasema neno "Chakari" au "Mwanamajiri"  linamaanisha "mnyongaji", kwa mfano ukipatikana na hatia kule gerezani kiasi cha kwamba umehukumumiwa kifo na imefika wakati wako wa kuuwawa, yule mtu atakayekunyoga ama atakayefuta kamba ili ufe anaitwa Chakari au Mwanamajiri. Lakini neno chakari linaweza kutumika katika sentensi na maana itakuwa tofouti, kwa mfano "Fulani amelewa chakari au amelewa chopi" linamaanisha umelewa sana kiasi kwamba ukitembea unakwenda kwa mazingira ya upepo..