Makumbusho hukuza jamii erevu- UNESCO

19 Mei 2017

Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya makumbusho yamefanyika hapo jana Mei 18, mwaka huu maudhui yakiwa ni  makumbusho na historia, kueleza kisichoelezwa, yakipigia chepuo jukumu la  makumbusho katika kukuza uhuru wa mawazo, na maarifa katika kuchangia jamii iliyoelimika.

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO linasema makumbusho ni miongoni mwa wabia muhimu katika ujenzi wa amani kwenye fahamu za wanaume na wanawake hususani katika werevu na kueleza utamaduni wa urithi wa asili.

Katika kuadhimisha siku hiyo UNESCO imetoa ujumbe wa video unaonyesha makumbusho na uritihi wa watu mbalimbali katika tamaduni tofauti.

( Sauti mchanganyiko)

‘‘Thomas ni mjerumani anasema katika utamaduni wake kuna kitu chaitwa Yodelling, wanafanya kama vile ililili, siwezi kuigiza vyema ni sauti ya ajabu…Huyu naye ni Preethi kutoka India anasema kuna kitu kinaitwa Charaminai katika mji mkongwe wa Hiderabad. Kijana huyu anatoka Niger, anasema kuna kitu kama ishara ya tatu karibu na kiuga cha bega ambayo ni ishara  ya kuangaza gizani.’’

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter