Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marufuku Pakistan kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya raia wa India : ICJ

Marufuku Pakistan kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya raia wa India : ICJ

Mahakama ya kimataiafa ya haki ICJ imeitaka Pakistan kufanya kila iwezalo isitekeleze hukumu ya kifo dhidi ya raia wa India Kulbhushan Sudhir Jadhav.

Mnamo mei 8, 2017, India ilifungulia kesi Pakistan ikipinga hukumu ya kifo dhidi ya raia huyo ambaye alihukumiwa adhabu hiyo akituhumiwa kuifanyia upelelezi Pakistan kinyume na sheria.

Taarifa ya ICJ inasema kwamba Pakistan inapaswa kutotekeleza adhabu ya kifo dhidi ya Jadhav, kufuatia umauzi wa mwisho, na inapswa kutoa taarifa kwa ICJ kuhusu utekelezaji wa amri hiyo.

Mahakama hiyo ya kimataifa ya haki imeongeza kuwa hadi itakapotoa uamuzi wa mwisho, hukumu hiyo itasubiri kulingana na amri hiyo.