Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

De Mistura atangaza kuanza kwa mchakato wa kitaalam katika mazungumzo ya Syria

De Mistura atangaza kuanza kwa mchakato wa kitaalam katika mazungumzo ya Syria

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Staffan de Mistura, ametangaza leo kuanza kwa mikutano ya kitaalam kati ya ujumbe wa serikali ya Syria na ofisi ya mjumbe huyo, wakimulika masuala ya mchakato wa katiba, zikiwemo kanuni za maisha.

Kufuatia tangazo hilo, ujumbe wa serikali ya Syria umetangaza kudhamiria kufanya mkutano mapema leo kati ya wataalam wake na wale wa Umoja wa Mataifa.

Mapema wiki hii, Bwana De Mistura alizifahamisha pande zote kuwa alinuia kuanzisha machakato wa kitaalam kushughulikia masuala ya katiba na sheria katika mazungumzo ya pande kinzani za Syria.