Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma ya Kangaroo yaimarisha usawa wa kijinsia Tanzania - UNICEF

Huduma ya Kangaroo yaimarisha usawa wa kijinsia Tanzania - UNICEF

Huduma ya kangaroo inayowezesha mtoto mchanga aliyezaliwa kabla ya muda wake kupata joto na kukua imekuwa muarobaini siyo tu katika kupunguza vifo vya watoto wachanga nchini Tanzania bali pia kuimarisha uhusiano wa kijinsia.

Dkt. Asia Hussein, meneja wa afya ya uzazi na mtoto , shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania amesema watoto hao hutakiwa kubebwa kifuani kwa saa 24 na hivyo kuwa karibu na mama na kwamba..

(Sauti ya Dkt. Asia-1)

Dkt. Asia akaenda mbali zaidi kuelezea ni kwa kipindi gani mtoto atabebwa kwa mtindo huo..

(Sauti ya Dkt. Aisha)