Hafla ya uvumbuzi na utandawazi katika kutimiza SDGs yafanyika UM

17 Mei 2017

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Peter Thomson, leo ameandaa hafla kuhusu uvumbuzi na utandawazi katika kuchukua hatua za kutimiza malengo ya maendeleo endelevu, kufuatia jukwaa la wadau mbali mbali kuhusu sayansi, teknolojia na uvumbuzi kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu .

Hafla hiyo imewaleta pamoja wavumbuzi wanaoongoza kutoka mashirika mbalimbali duniani na nchi wanachama, kujadili jinsi teknolojia zinazoibuka zinavyoweza kuendeleza juhudi za kutimiza Ajenda yam waka 2030 na ndipo Bwana Thomson akafunguka.

(Sauti ya Thomson)

“Mnavyofahamu, kikao cha 71 cha Baraza la Umoja wa Mataifa kinajikita zaidi katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu. Hii ni sehemu ya msururu wa hafla za kuchukua hatua kuhusu SDGs. Leo, hasa ni kuhusu kuelekeza akili zetu katika jinsi gani tunaweza kutumia ukuaji mkubwa wa uvumbuzi, teknolojia na utandawazi katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu.”

Naibu Katibu Mkuu, Amina Mohamed amezungumza kwenye hafla hiyo, akisema uvumbuzi utumike kuchagiza SDGs, akiangazia kutokomeza umaskini na malengo mengine, akisema....

(Sauti ya Amina)

 ''Tunafikiri kwamba malengo haya yatafikia miisho ya dunia yanakotakiwa,  kila kona ya nchi, na visiwa kwa ajili ya ubia. Ubia ambao unahitajika ili kutimiza hili.''

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter