Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lakutana kujadili hali Somalia

Baraza la Usalama lakutana kujadili hali Somalia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekuwa na kikao kuhusu hali nchini Somalia, ambapo limehutubiwa na Bwana Raisedon Zenenga, Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM.

Katika hotuba yake, Bwana Zenenga amesema baa linalotokana na ukame nchini Somalia bado linaendelea, na kwamba hali ya kibinadamu imezorota kasi zaidi kuliko ilivyotarajiwa, tathmini zilizofanywa mwezi Aprili zikionyesha viwango vya kutia wasiwasi vya unyafuzi.

Ametoa wito kwa wadhamini wa kimataifa waongeze usaidizi wao kwani mzozo wa kibinadamu Somalia hauonyeshi dalili za kumalizika sasa, lakini pia hatua zichukuliwe kuifanya Somalia kuwa thabiti zaidi.

(Sauti ya Senenga)

« Somalia itaendelea kusonga kutoka mzozo mmoja unaoweza kuepukika hadi mwingine, iwapo uthabiti hautaimarishwa kwa kushughulikia matatizo ya taifa ya kimfumo. Kuwekeza katika kuongeza uwezo wa taasisi za kitaifa na mikakati inayolenga maendeleo inapaswa kupewa kipaumbele katika kuisaidia nchi kuhimili vyema zaidi mizozo ya kibinadamu siku zijazo. »