EU thabiti ni muarobaini wa matatizo- Guterres

17 Mei 2017

Akiwa Strasbourg nchini Ufaransa baada ya kuhutubia Bunge la Ulaya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema mshikamano thabiti baina ya nchi za Muungano wa Ulaya ndio muarobaini wa suala la wakimbizi linalogubika ukanda huo hivi sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari, amesema baadhi ya nchi zimetindikiwa idadi kubwa ya wakimbizi na hivyo kushindwa kuwapatia huduma zenye utu akisema..

(Sauti ya Guterres)

“Mshikamano unaweza kutatua shida zote. Bila mshikamano kuacha nchi moja tu, tena bila shaka zile ambazo wakimbizi wanaingia kwanza ziko katika hali ngumu sana. Kuacha nchi moja pekee, itakuwa vigumu sana kutatua tatizo.”

Bwana Guterres amesisitiza pia mshikamano wa kikanda na kimataifa kuwezesha kumaliza vita na mizozo, kusaidia wakimbizi wa ndani kwenye nchi zao na pia kusaidia nchi ambako wamekimbilia.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter