Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO/IAEA kutathimini udhibiti wa wadudu ikiwemo kuwafanya tasa

FAO/IAEA kutathimini udhibiti wa wadudu ikiwemo kuwafanya tasa

Shirika la kimataifa la nguvu za atomiki (IAEA) litakuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa kudhibiti wadudu wanaoeneza magonjwa na kuathiri mazao duniani.

Mkutano huo wa tatu wa kimataifa utakaojumuisha pia matumizi ya mbinu ya kuwafanya wadudu kuwa tasa na mbinu zingine zinazotumia nyuklia, unaandaliwa kwa pamoja na shirika la chakula na kilimo, FAO na utaanza Mei 22 hadi 26 mjini Vienna, Austria.

Wataalamu wa kimataifa 400 katika nyanja za kilimo, entomolojia, jeni na afya ya umma, watakusanyika kutathmini mitazamo ya sasa, mwenendo na changamoto zinazosababishwa na wadudu na tishio lao kwa kilimo na afya ya wanyama na binadamu.

Mada zingine zitakazogusiwa ni pamoja na athari za kusambaa kwa wadudu kama mabadiliko ya tabia nchi na biashara ya kimataifa.