Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF atembelea Tanzania

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF atembelea Tanzania

Tanzania imeliomba shirika la fedha duniani, IMF isaidie kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu na uwekezaji katika sekta ya viwanda.

Rais John Magufuli amesema hayo Jumanne jijini Dar es salaam wakati wa mazungumzo yake na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF Tao Zhang aliyetembelea nchi hiyo.

Magufuli amesema kwa sasa nchi hiyo ya Afrika Mashariki inatekeleza mpango wa pili wa maendeleo utakaowezesha kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, hivyo usaidizi wa IMF utachagiza utekelezaji.

Kwa upande wake Bwana Tao amesema uchumi wa Tanzania umeendelea kukua na kwamba mwelekeo huo unachagizwa na sera na mageuzi katika sekta ya uchumi.

Amesema ni matumaini yake kuwa iwapo serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo itaweza kukabiliana na changamoto mbali mbali za kiuchumi zinazokumba dunia hivi sasa.