Maisha bora nyumbani kivutio kwa wakimbizi kurejea makwao

16 Mei 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR katika kushughulikia suala la wakimbizi lina mikakati mitatu. Mosi ni wale walioko ukimbizi kupatiwa uraia, pili walioko ukimbizini kuhamishiwa nchi ya nyingine ya tatu na mpango wa mwisho ni wakimbizi kurejea makwao pindi hali inaporuhusu. Vigezo vya kurejea nyumbani ni pamoja na hali ya usalama na fursa za kuwawezesha wakimbizi kujikimu wao na familia zao. Nchini Myanmar, mazingira bora nyumbani na fursa za ajira zimewezesha wakimbizi kuanza kurejea nyumbani baada ya kuishi ukimbizi kwa zaidi ya miaka 10. Mmoja wao ndiye maudhui makuu ya makala hii kama inavyosimuliwa na Assumpta Massoi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter