Microsoft yapigia chepuo haki za binadamu

16 Mei 2017

Ushirika wa aina yake wa miaka mitano baina ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa na kampuni ya teknolojia ya Microsoft umetangazwa Jumanne mjini Geneva Uswis.

Kama sehemu ya ushirika huo kampuni ya Microsoft itatoa dola milioni 5 kusaidia kazi za ofisi ya haki za binadamu.

Ofisi hiyo inasema wakati jamii duniani zikiendelea kukabiliwa na changamoto za haki za binadamu ushirika huu utaainisha umuhimu wa matumizi ya teknolojia kusaidia kukabiliana na changamoto hizo na kutoa fursa kwa sekta binafsi kusaidia kazi za ofisi ya haki za binadamu. Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RAVINA)

“Ushirika huo utajikita katika maendeleo na matumizi ya teknolojia ya juu iliyoundwa ili kutabiri, kuchambua na kukabiliana na hali ngumu za haki za binadamu, ambazo kwa sasa zinaonekana si tu zinaongezeka katika maeneo mengi ya dunia ikiwa ni pamoja maeneo ambayo awali yalionekana kama imara, lakini pia kuongezeka kwa utata wa hali hizo"

Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni binafsi kutoa kiwango hicho cha msaada kusaidia masuala ya ofisi ya haki za binadamu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter