Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

China yaipiga jeki IOM kusaidia Somalia

China yaipiga jeki IOM kusaidia Somalia

Shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Uchina wametia saini makubaliano kwa ajili ya kuisaidia Somalia.

Muafaka huo uliotiwa saini Mai 15 baina ya mkurugenzi mkuu wa IOM William Lacy Swing, na wizara ya fedha ya Uchina, ni wa dola miliioni moja ambazo zitasaidia juhudi za IOM za kutoa msaada Somalia kwa wakimbizi wa ndani, watu wasiojiweza na Wasomali wanaorejea nyumbani.

Balozi Swing amekaribisha mchango huo wa China ambao ni wa kwanza kabisa tangu taifa hilo kuwa mwanachama wa 165 wa IOM mwezi Juni mwaka 2016.