Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visa vinavyoshukiwa vya Ebola vyaongezeka DRC

Visa vinavyoshukiwa vya Ebola vyaongezeka DRC

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC idadi ya visa vinavyoshukiwa kuwa ni Ebola imeongezeka na kufikia 20.

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema kati ya visa hivyo shukiwa, visa viwili vimethibitishwa katika maabara ya taifa kuwa ni Ebola na idadi ya waliofariki dunia imesalia kuwa ni watu watatu.

Msemaji wa WHO mjini Geneva, Uswisi, Christian Lindmeier amesema jopo la wataalamu wa afya kutoka wizara ya afya nchini DRC linaendelea na uchunguzi huko Likati kwenye jimbo la Bas-Ulele kwa ushirikiano na wataalamu wa shirika hilo na kwamba..

(Sauti ya Christian)

“Hivi sasa kuna watu 400 wanaofuatiliwa kwa uchunguzi kwenye maeneo manne tofauti, na sampuli mpya tano zimekusanywa tayari na punde zitafanyiwa uchunguzi.”