Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame waibua maradhi kwa raia Somalia

Ukame waibua maradhi kwa raia Somalia

Kulingana na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, takriban watu 22,000 wameripotiwa kukumbwa na maradhi kama utapiamlo, kipindupindu na kuhara damu nchini Somalia kufuatia ukame uliokithiri.

Mji wa Baidoa ni moja wa maeneo ulioathiriwa zaidi. Katika makala ifuatayo, Selina Jerobon anaangazia hali  halisi katika moja ya hospitali za Baidoa, ambako wanawake,wanaume na watoto  waanakabiliana na madhila ya ukame. Ungana naye..