Baraza la usalama lajadili ukatili wa kingono vitani

15 Mei 2017

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limejadili ajenda kuhusu wanawake na amani na usalama na uhusiano wa dhana hiyo katika ukatili wa kingono kwenye maeneo yenye migogoro. Joshua Mmali na taarifa zaidi.

( TAARIFA YA JOSHUA)

Miongoni mwa waliohutubia mkutano huo ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohamed ambaye ametumia muda mwingi wa hotuba yake kuelezea juhudi za jumuiya ya kimataifa na taasisi mbalimbali katika kukabiliana na ukatili wa kingono katika maeneo ya kivita.

Kiongozi huyo amesema licha juhudi hizo ukatili wa kingono na usafirishaji haramu wa kibinadamu sasa umechukua sura mpya kwani magaiadi na watu wenye kigaidi na misimamo mikali hutumia uhalifu huo kama ngome.

Suala la kuachiwa kwa watoto wa Chibok nchini Nigeria likachomoza ambapo licha ya kupongezwa juhudi hizo Naibu Katibu Mkuu ameonya.

( Sauti Amina)

‘‘Haitoshi kuwarejesha watoto wetu, lazima tuwarejeshe kwa utu na heshima. Katika mazingira ya usaidizi, usawa na fursa, na kuhakikisha wanapatiwa usaidizi wa kisaikolojia. Wahanga wa ukatili wa kingono pia wana haki ya mpango madhubuti wa fidia.’’

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter