Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali ya wanafunzi Tanzania na mustakhbali wa usalama barabarani

Ajali ya wanafunzi Tanzania na mustakhbali wa usalama barabarani

Tarehe 8 hadi 14 mwezi huu wa Mei ni wiki ya usalama barabarani duniani. Shirika la afya ulimwenguni, WHO ambayo ndiyo mratibu wa siku hii imeeleza bayana kuwa hali ya usalama barabarani licha ya kuimarika katika baadhi ya nchi, hali inazidi kuwa mbaya Afrika, Asia na Amerika ya Kusini ambako ongezeko la magari haliendi sambamba na usimamizi wa sheria na kanuni za usalama barabani, watu zaidi ya milioni 1.2 wakipoteza maisha kila siku barabarani sababu ikiwemo kutokuvaa mikanda na mwendo kasi. Leo hii basi tunaangazia Tanzania ambako wiki ya usalama barabarani iligubikwa na msiba wa vifo vya watu 36 vilivyotokana an ajali ya barabarani mkoani Arusha, kaskazini mwa nchi hiyo wengi wao wanafunzi wa shule ya msingi. Mwenyeji wetu ni Nicolaus Ngaiza, wa radio washirika Kasibante FM ya mkoani Kagera!