Skip to main content

Hatua madhubuti zahitajika kutekeleza Mkataba wa Paris na SDGs – Amina Mohamed

Hatua madhubuti zahitajika kutekeleza Mkataba wa Paris na SDGs – Amina Mohamed

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohamed, amesema nchi ni lazima zichukue hatua madhubuti haraka kutimiza malengo ya Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi, na kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa sababu fursa ya kufanya hivyo inazidi kuwa finyu.

Bi Mohamed alikuwa akihutubia jukwaa la nishati jijini Vienna, Austria, ambako wawakilishi kutoka sekta mbalimbali kote duniani wamekusanyika kujadili masuala muhimu katika mjadala kuhusu nishati.

(SAUTI AMINA)

“Tukiwa na azma ya kuchukua hatua, tunaweza kutimiza malengo la Mkataba wa Paris na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu, na kuwezesha ufanisi kwa mabilioni ya watu. Lakini tunapaswa kuchukua hatua haraka, na kwa njia madhubuti, kwani fursa hiyo inazidi kuwa finyu.”

Mwaka huu, jukwaa hilo la nishati linamulika utimizaji wa nishati endelevu kwa ajili ya kutekeleza SDGs na Mkataba wa Paris, ambao unalenga kudhibiti ongezeko la joto duniani na kuhakikisha linasalia chini ya nyuzi joto mbili.