Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa masuala ya bahari utakuwa kipimo cha utekelezaji SDG 14-UNCTAD

Mkutano wa masuala ya bahari utakuwa kipimo cha utekelezaji SDG 14-UNCTAD

Mkutano wa kimataifa wa masuala ya bahari unaotarajiwa wiki chache kutoka sasa hapo juni 5-7 utakuwa ni kipimo cha utashi wa kisiasa kwa nchi, mashirika, asasi za kiraia na wadau wengine katika kuhakikisha utekelezaji wa lengo nambari 14 la maendeleo endelevu yaani SDGs.

Kauli hiyo imetolewa Jumatano mjini Geneva Uswisi na Lucas Assuncao mkuu wa biashara, mazingira, mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu kwenye idara ya biashara ya Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD.

Akizungumzia umuhimu wa mkutano wa bahari na SDG 14 lengo linalogusia maisha ya viumbe chini ya maji, amesema inafahamika kwamba uvuvi hasa wa samaki unafanyika katika njia ambayo sio endelevu mfano kwenye bahari ya mediterenia na black sea ambako asilimi 9-70 ya samaki huvuliwa kiwango cha kupindukia hali ambayo inahatarisha utekelezaji wa lengo hilo. Na kuhusu kwa nini UNCTAD inajuhusisha na suala hilo, Lucas amesema

(SAUTI YA LUCAS)

"Kwa sababu ni dhahiri kwamba soko la kimataifa la bidhaa za uvuvi ni dola bilioni 146 kwa mwaka, kutokana na haja kubwa ya biashara ya bidhaa hizo inayokuwa kwa kasi, mahitaji yanasalia kuwa makubwa na hasa ukanda wa Asia, tuna wasiwasi sana kuhusu soko hilo sawia na lile la kimataifa , na hilo ni tatizo hivyo ni kitu kizuri cha kimataifa lakini hakinufaishi sawia nchi zote zenye bahari.”