Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP na wadau wahaha kusaidia CAR inapokumbwa na mzozo wa kibinadamu

WFP na wadau wahaha kusaidia CAR inapokumbwa na mzozo wa kibinadamu

Tangu machafuko yalipozuka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), taifa hilo limejikuta katika mzozo wa kibinadamu unaoendelea. Lakini mzozo wa nchi hiyo ni moja ya mizozo ya kibinadamu iliyosahaulika ulimwenguni, na kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Chakula Ulimwenguni (WFP), ufadhili kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu unazidi kudidimia. Kwa mfano, WFP inasema mpango wake wa shughuli za kibinadamu kwa mwaka 2017, umefadhiliwa kwa asilimia saba tu kufikia sasa.

WFP na wadau wake wa kibinadamu wameonya kuwa, kuupuuza mzozo wa kibinadamu wa CAR huenda kukaiweka nchi hiyo katika hatari ya kutumbukia katika machafuko tena, ambayo athari zake zitavuka mipaka. Kwa mengi zaidi, ungana na Joshua Mmali katika makala ifuatayo.