Japan ni mfano wa kuigwa kimataifa kwa lishe bora-FAO

Japan ni mfano wa kuigwa kimataifa kwa lishe bora-FAO

Japan ina utamaduni wa kipekee wa chakula ambao unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuboresha lishe kimataifa amesema Jumatano  mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO anayezuru nchini hiyo. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Graziano da Silva amesema Japani ni mfano wa kuigwa kwa lishe bora , kwa sasa ikiwa na kiwango kidogo cha matatizo ya utipwatipwa miongoni mwa nchi zilizoendelea ambacho ni chini ya asilimia 4.

Amesema utamaduni huo wa kipekee wa chakula unajumuisha matumizi makubwa ya mboga za majani, matunda na samaki na hasa wakitumia utaalamu wa Washoku ambao ni ujuzi wa uaandaji na ulaji wa mlo uliotajwa kwenye orodha ya shirika la elimu sayansi na utamaduni UNESCO kama ni urithi wa kitamaduni usiogusika.

Amesema sheria na sera zinazotumika Japan katika kuchagiza lishe bora zinaweza kuigwa na nchi nyingine hasa katika kuelimisha watoto na kudhibiti utipwatipwa.