Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi mwema wa ILO uso kwa uso nawahanga wa utumwa wa kazi

Balozi mwema wa ILO uso kwa uso nawahanga wa utumwa wa kazi

Balozi mwema wa shirika la kazi duniani ILO,Wagner Moura, amekutana uso kwa uso na kwa mara ya kwanza na waliokuwa wahanga wa utumwa mamboleo nchini Brazil mapema mwezi huu.

Shirika la kazi duniani hapo jana limezindua kampeni ya siku 50 ya uhuru dhidi ya utumwa makazini.

Miongoni mwa waliokutana na balozi mwema huyo ni Rafael Ferreira ambaye alilazimishwa kufanya kazi katika shamba na alilazimika kufanya hivyo ili alipe deni la babake. Ferreira ameeleza kuwa hali kwa watumwa wa kazi ni tete na hulazimika kufanya kazi mufululizo.

Kwa sasa Ferreira anasoma uhandisi chuoni.

Balozi mwema Moura, ambaye kwa mwaka mmoja amekuwa akitetea kukomeshwa kwa utumwa kazini amesema ameanza harakati zake tangu utoto aliokuwa katika mji uitwao Bahia chini humo aliposhuhudia visa vingi lakini wakati huo aliamaini kwamba ni sahihi.

Amesema alipobaini kuwa wafanyakazi wana haki za binadamu na zinapaswa kuheshimiwa hapo ndipo maisha yalibadilika na kuanza harakati dhidi ya vitendo hivyo .