Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maldives chunguza mauaji ya mwanahabari- Wataalamu

Maldives chunguza mauaji ya mwanahabari- Wataalamu

Mamlaka nchini Maldives zitekeleze wito wa Rais Abdulla Yameen Abdul Gayoom wa kuchunguza mauaji ya mwanahabari mashuhuri, bloga na mtetezi wa haki za binadamu nchini humo Yameen Rasheed.

Tamko hilo limetolewa na wataalamu maalum watatu wa Umoja wa Mataifa David Kaye, Michel Forst na Ahmed Shaheed ambapo pamoja na kulaani mauaji hayo ya tarehe 23 mwezi uliopita, wametaka Maldives ichukue hatua kulinda haki ya watu kujieleza kwa uhuru.

Mwanahabari Rasheed alikuwa ameuawa kwa kuchomwa visu nyumbani kwake huko Malé katika kisa ambacho ni mfululizo wa mashambulizi dhidi ya wanahabari na watetezi wa haki wanaoeleza wazi mawazo yao.

Rasheed alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali na maandiko yake kuhusu tuhuma za rushwa dhidi ya serikali yamedaiwa kumsababishia kupata vitisho vya kuuawa, vitisho ambavyo licha ya kuripoti polisi hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Wametaka uchunguzi wa kisa hicho na vinginevyo uwe huru.