Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuukabili mwendokasi kwa mikakati minne-WHO

Tuukabili mwendokasi kwa mikakati minne-WHO

Wiki ya usalama barabarani ikiwa imeng’oa nanga hapo jana, jamii ya kimataifa imetakiwa kukabiliana kwa nguvu zote na moja ya vyanzo vikuu vya ajali za barabarani ambacho kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO ni mwendo kasi.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Margaret Chan amesema hatua nne rahisi zapaswa kuchukuliwa hima katika miji na vijiji ili kukabiliana na mwendokasi ambayo ni.

(Sauti Chan)

‘‘Kuanzisha vizuizi vya kupunguza mwendokasi kama vile matuta ya barabarani, kuanzisha na kutekeleza sera ya viwango vya mwendo, kuweka teknolojia katika magari kama vile breki za dharura, na la mwisho lililo muhimu ni kuelimisha watu kuwa mwendokasi unaua.’’

Theluthi moja ya vifo vya ajali za barabarani husababishwa na mwendokasi zikiathiri zaidi maisha ya vijana kati aya maika 15 hadi 29.

WHO inasema ajali za barabarani ni chanzo kikuu cha vifo kwa vijana katika umri huo.

Katika kampeni ya wiki ya usalama barabarani, WHO imeweka wavuti maalum inayoonyesha sheria za barabarani kuhusu mwendo kasi ziko namna gani katika kila nchi duniani na iwapo zinakidhi viwango au la.