Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunakaribisha kuachiliwa kwa wasichana wa Chibok lakini bado tuna hofu:UM

Tunakaribisha kuachiliwa kwa wasichana wa Chibok lakini bado tuna hofu:UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António  Guterres amesema ingawa anakaribisha kuachiliwa huru kwa wasichana 82 wa Chibok kutoka kwa kundi la Boko Haram lakini bado Umoja wa Mataifa unahofia usalama na mustakhbali wa wasichana wengine wa shule na watu ambao bado wanashikiliwa na kundi hilo.

Kupitia taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa Wanigeria wote ikiwemo familia na jamii za wasichana walioachiliwa kuwapokea katika jamii na kuwapa msaada wowote wanaouhitaji ili kuhakikisha wanajiunga kikamilifu tena na jamii hizo. Na kuongeza

(SAUTI YA STEPHANE)

“Pia tunaitaka jumuiya ya kimataifa kuendelea kuisaidia serikali ya Nigeria katika juhudi za kuhakikisha usaidizi na ujumuishwaji wa waathirika wote wa kundi la Boko Haram”

Wasichana zaidi ya 200 wa shule ya Chibok walitekwa na kundi la Boko Haram mwezi Aprili mwaka 2014.