Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgogoro DRC wawaacha watoto milioni mbili na unyafuzi

Mgogoro DRC wawaacha watoto milioni mbili na unyafuzi

Karibu watoto milioni mbili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, wenye umri chini ya miaka mitano wana unyafuzi kutokana na machafuko yanayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva hii leo mkuu wa operesheni za Umoja wa Mataifa zilizo chini ya ofisi ya umoja hiyo ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, Rein Paulsen amesema nchini DRC hali ya kibinadamu ni mbaya kwani katika kipindi cha miezi mitano iliyopita kumekuwa na ongezeko la watu milioni 3.7 waliofurushwa.

Amesema mapigano ya kikabilla yanaripotiwa kila uchao katika majimbo mbalimbali ikiwamo Kasai.

( Sauti Rein)

‘‘Niko hapa pia kusema kwamba pamoja na kuzindua ombi la usadizi kwa ajili ya Kasai, tunachohitaji ni juhudi za pamoja za usaidizi kwa DRC kwa ujumla. Mgogoro huu unakuwa sio tu kwa idadi lakini pia kijografia.’’