Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wawasili Ulaya kupitia Mediteranean mwisho wa wiki-Grandi

Maelfu wawasili Ulaya kupitia Mediteranean mwisho wa wiki-Grandi

Zaidi ya watu elfu 6,000 wamevuka bahari ya Mediterranean Kutoka Afrika ya Kaskazini na kuingia Italia tangu Ijumaa, katika safari ya hatari ambayo haipaswi kuendelea amesema mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. John Kibego na taarifa kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Filippo Grandi amesema idadi hiyo ya Jumamosi imefanya jumla ya wakimbizi na wahamiaji 43,000 waliovuka bahari hiyo kwa mwaka huu pekee huku watu wengine zaidi ya elfu moja ama wametoweka au kufa maji, ikiwa ni mtu mmoja kati ya kila watu 35 wanaojaribu safari hiyo ya hatari.

Ameongeza kuwa wengi wa watu hao wanakimbia vita na machafuko Afrika na Mashariki ya Kati, au wanasaka maisha bora kwa ajili yao na familia zao. Grandi amesikitishwa na kiwango cha ukatili wa wasafirishaji haramu na kusema kuna haja ya haraka ya kushughulikia mizizi ya matatizo ya wahamiaji na wakimbizi na kuwapa njia mbadala wanaohitaji ulinzi.

Mwaka jana watu 46,000 waliokolewa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean.