Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasafirisha mamia ya wakimbizi wa Sudan Kusini kuingia Ethiopia

IOM yasafirisha mamia ya wakimbizi wa Sudan Kusini kuingia Ethiopia

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limeanza kuwasafirisha wakimbizi wa Sudan Kusini kutoka eneo la Pagak la mpakani mwa Ethiopia jimbo la Gambella na kuwapeleka kwenye kambi ya wakimbizi ya Gore-Shembola iliyoko jimbo la Benishangul Gumuz ndani ya Ethiopia.

Kufuatia mapigano ya karibuni na uhaba wa chakula Sudan Kusini vilivyochangia hali kuwa mbaya zaidi, IOM inasema wakimbizi wengine 30,000 wanatarajiwa kuingia Gambella katika miezi michache ijayo.

Kambi ya Gambella, moja ya maeneo masikini kabisa Ethiopia imeelezwa kufikia pumwani mwa uwezo wake huku idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini ikipita ile ya wenyeji.