Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaelekeza usaidizi kwa wahanga wa tetemeko la ardhi Tanzania

FAO yaelekeza usaidizi kwa wahanga wa tetemeko la ardhi Tanzania

Shirika la kilimo na chakula duniani, FAO limezindua mradi wa uwezeshaji wananchi katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji mkoani Kagera kaskazini magharibi nchini Tanzania, kama njia ya kuimarisha uhakika wa chakula baada ya tetemeko la ardhi mwezi Septemba mwaka jana.

Mradi huo wenye thamani ya dola 299,000, umeanza kutekelezwa mwezi Aprili mwaka huu na utaendelea hadi januari 2019, kwenye halmashauri tano za mkoa huo, ukilenga kuwafikia watu elfu tano wakiwemo wakulima, wavuvi na wafugaji.

Mshauri wa masuala ya kilimo kutoka shirika la chakula FAO Deomedes Kaliisa, amesema wamechukua hatua hiyo kufuatia tathmini ya pamoja na serikali iliyofanywa mwezi Oktoba mwaka jana.

(Sauti ya Kaliisa)

Naye Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jeneral mstaafu Salum Kijuu, ameshukuru akisema mradi umekuja wakati muafaka.

(Sauti ya Meja Jenerali mstaafu Kijuu)