Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Panda mti kibiashara ni mkombozi wa misitu Tanzania- Dkt. Mwakalukwa

Panda mti kibiashara ni mkombozi wa misitu Tanzania- Dkt. Mwakalukwa

Sera ya ushirikishaji jamii katika uhifadhi wa misitu  nchini Tanzania imezaa matunda na sasa wananchi pamoja na kulinda misitu iliyo jirani nao wameweza kupata manufaa kwa kuuza baadhi ya mazao ya misitu. Mpango huo umekuwa moja ya mafanikio ya harakati za Tanzania za kulinda misitu kwa uendelevu kwa mujibu wa malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs. Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki kwenye Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania Dokta Ezekiel Mwakalukwa ambaye anashiriki mkutano wa misitu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani amemweleza Assumpta Massoi wa Idhaa hii kuwa ingawa kuna changamoto bado sera hiyo imezaa matunda ambapo anaanza kwa kuelezea jinsi sera hiyo inavyofanya kazi.