Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakandarasi wawasili Sudan Kusini kusaidia ujenzi wa miundombinu

Wakandarasi wawasili Sudan Kusini kusaidia ujenzi wa miundombinu

Kikosi cha askari 35 kutoka Uingereza kimewasili Juba, makao makuu ya Sudan Kusini kuungana na wakandarasi wenza wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS.

Akizungumza baada ya kuwasili, Kamanda wa kikosi hicho Luteni Colonel Jason Ainley amesema vikosi zaidi vinatarajiwa kuwasili na kufanya idadi kuwa karibu 400 kutoka 230 ya sasa.

Luteni Ainley ameeleza wajibu wa kikosi.

(Sauti Luteni Ainley)

‘‘Kimsingi tutakuwa hapa kuimarisha usalama wa mioundombinu, yaweza kuwa malazi, uzio wa usalama, barabara na mifereji. Miradi tunayoilenga ni kuimarisha maeneo ya kutua helikopta huko Makakaal na Bentiu na zaidi kuimarisha eneo la kutua ndege Malakaal ambayo ni njia muhimu ya kupeleka mahitaji kwa idara za Umoja wa Mataifa na misaada ya kibinadamu.’’

Idadi hii ya kikosi cha askari 400 itakuwa miongoni mwa vikosi vyenye idadi ya watu wengi zaidi kutoka Uingereza kupelekewa kwenye maeneo ya operesheni.