Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili wa Denmark kusaidia ukame Pembe ya Afrika na Sudan kusini

Ufadhili wa Denmark kusaidia ukame Pembe ya Afrika na Sudan kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limekaribisha ufadhili wa dola milioni 10.7 kutoka serikali ya Denmark ili kukabiliana na baa la njaa Sudan  Kusini na kusaidia maelfu ya watu wanaokabiliwa na njaa kutokana na ukame kwenye Pembe ya Afrika. Tarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

WFP inaishukuru sana Denmark kwa msaada huo amesema Valarie Guarnieri mkurugenzi wa WFP wa kanda ya Afrika Mashariki na Kati , akiongeza kuwa kuokoa maisha ya watu sasa kabla hali haijawa mbaya zaidi kutapunguza hatari ya vifo na gharama, ikilinganishwa na kuchukua hatua wakati tumeshachelewa na watu wengi wameshapoteza maisha.

Naye waziri wa ushirika na maendeleo wa Denmark Ulla Tørnæs akikabidhi msaada huo amesema endapo jumuiya ya kimataifa haitochukua hatua sasa ukame Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika utaishia kuwa janga la kimyakimya litakalogharimu maisha ya maelfu ya watu, akiongeza kuwa hii ndio sababu Denmark inachukua hatua sasa kwa ajili ya kunusuru maisha ya watu nchini Somalia, Sudan Kusini, Ethiopia na Kenya .