Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya samaki jodari duniani

Leo ni siku ya samaki jodari duniani

[caption id="attachment_316858" align="aligncenter" width="615"]jodariday

Nchi nyingi duniani hutegemea rasilimali za samaki aina ya jodari au maarufu kama tuna kwa ajili ya uhakika wa chakula, lishe, maendeleo ya kiuchumi, ajira, mapato ya serikali, maisha, utamaduni na burudani.

Katika kuadhimisha kwa mara ya kwanza kabisa siku ya jodari au tuna duniani Mei pili, shirika la chakula na kilimo FAO linasema hivi sasa zaidi ya nchi 80 zinafanya uvuvi wa jodari, maelfu ya boti za uvuvi wa jodari zimesheheni na uwezo wa uvuvi wa samaki hao unaongezeka katika bahari ya Hindi na Pacifiki.

Siku hii inaadhimishwa ili kuainisha umuhimu udhibiti endelevu wa samaki katika kufikia ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030.

Siku hii ilipitishwa na azimio la baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2016.