Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi mtendaji wa WFP yuko ziarani Syria na Lebanon:

Mkurugenzi mtendaji wa WFP yuko ziarani Syria na Lebanon:

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP, David Beasley, anazuru Lebanon na Syria , kukutana na raia wa Syria walioathirika na mgogoro unaondelea lakini pia kushuhudia hali halisi.

Beasley ambaye amekuwa ziarani tangu Aprili 30 hadi Mai 3 anakutana pia na maafisa wa serikali na wadau wengine kujadili operesheni za kibinadamu katika nchi zote mbili ambako WFP inatoa msaada wa chakula na fedha, lakini pia kukutana na wafanyakazi wa shirika hilo.

Tangu kuzuka kwa mzozo wa Syria miaka sita iliyopita WFP imekuwa msitari wa mbele kusaidia mamilioni ya waathirika ndani ya Syria, Lebanon na katika kanda nzima. Kila mwezi WFP inatoa msaada kwa takribani wakimbizi 700,000 wa Syria walioko Lebanon kupitia vocha za chakula.