Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wamasai ni wakati wakubadilika katika ufugaji: Martha Ntoipo

Wamasai ni wakati wakubadilika katika ufugaji: Martha Ntoipo

Wakati mkutano wa 16 wa watu wa asili ukiendelea mjini New York Marekani, jamii hizo zinazojihusisha na ufugaji hususani wamasai zimetakiwa kubadilisha mfumo wa ufugaji ili kupata maendeleo endelevu, amesema Martha Ntoipo mwakilishi wa jamii ya wafugaji nchini Tanzania kutoka taasisi ya wafugaji na maendeleo (PIDO).

Katika mahojiano maalum na idhaa hii, Bi Martha amesema jamii ya Kimasai inaweza kupiga hatua zaidi kupitia ufugaji akisema.

( Sauti Martha)

Bi Ntoipo amesema baada ya mkutano huu atahakikisha jamii asilia zinapata taarifa ya kile kilichojiri kwa kutumia mkakati huu.

( Sauti Martha)