Guterres atiwa wasiwasi na ongezeko na mvutano wa kijeshi DPRK

28 Aprili 2017

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, ameliambia baraza la usalama Ijumaa kwamba anatiwa wasiwasi na hatari ya kuongezeka mvutano wa kijeshi dhidi ya mipango ya nyuklia ya Jamhuri ya watu wa Korea au DPRK.

Ameonya dhidi ya hatari ya "upangaji mbovu au kutokuelewa" kwa upande wa jamii ya kimataifa na kusema kuna haja ya kupunguza mvutano dhidi ya DPRK, ambayo kwa kawaida hujulikana kama Korea ya Kaskazini.

Katibu mkuu amelaani vikali DRK kuelendea kukiuka mara kwa mara maazimio ya baraza la usalama ambayo yanalenga kudhibiti shughuli za nyuklia na makombora nchini humo.

Tangu Januari mwaka jana Korea ya Kaskazini imefanya majaribuo mawili ya nyuklia na kurusha makombora zaidi ya 30. Guterres amesema nia ya DPRk kuunda sialaha za nyuklia ni tishio la dhahiri kwa ukanda mzima na usalama wa kimataifa , na inaathiri juhudi za kimataifa za kupambana na silaha hizo.

Lakini ametoa wito kwa nchi wanachama kumakinika wanapokabiliana na tishio hilo.

(SAUTI YA GUTERRES)

“nitatiwa wasiwasi na hatari ya kuendelea kwa mvutano wa kijeshi katika kanda ikiwemo mipango mibovu au kutoelewa. Wajibu ni kwa DPRK kuzingatia majukumu yake ya kimataifa. Wakati huo huo, jumuiya ya kimataifa lazima pia iongeze jitihada za kusimamia na kupunguza mvutano.”

Katibu Mkuu ameongeza kuwa hatua zinahitajika sasa ili kuzuia migogoro na kufikia amani ya kudumu na ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kusaidia takribani raia milioni 13 wa Korea Kaskazini wanaohitaji msaada ambao ni nusu ya watu wa taifa hilo.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter