Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatimiliki huwezesha ubunifu kunufaisha jamii-WIPO

Hatimiliki huwezesha ubunifu kunufaisha jamii-WIPO

Aprili 26 ni siku ya hatimiliki duniani ambako katika kuadhimisha siku hii Mkurugenzi mkuu wa  shirika la kimataifa la hatimiliki, WIPO, Francis Gurry amesema, hatimiliki ni sehemu muhimu ya sekta ya ubunifu na ina faida kwa wale wanaochukua fursa ya kuzindua bidhaa mpya na huduma katika uchumi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Ubunifu- kuimarisha maisha” ambako Bwana Gurry amesema licha ya kwamba ubunifu unaimarisha maisha yetu, mara nyingi jamii haichukui muda kutafakari jinsi ubunifu ulivyobadilisha kiwango cha maisha.

Aidha ameongeza kwamba ukilinganisha maisha yalivyokuwa karne moja iliyopita kuna tofauti kubwa katika kiwango cha maisha kufuatia uwepo wa bidhaa nyingi za ubunifu.

Licha ya kwamba ubunifu huu una fadia chungu nzima kwa bindamu lakini, pengo katika ulinzi wa hatimiliki bado ni changamoto katika baadhi ya nchi. Basi ungana na Joseph Msami katika ripoti hii