Takwimu za vifo, majeruhi kazini zitasaidia kumarisha usalama: ILO

Takwimu za vifo, majeruhi kazini zitasaidia kumarisha usalama: ILO

Leo ni siku ya usalama na afya kazini duniani, shirika la kazi duniani ILO linasema kuna umhimu wa dharura wa kumarisha usalama na afya katika ameno ya kazi ili kupunguza idadi ya majeruhi na vifo vitokanavyo na ajali kazini.

Katika taarifa yake ILO inasema kuwa vifo milioni 2.3 na ajali milioni 300 ambazo zimesababisha majeruhi hutokea katika maeneo ya kazi kila mwaka, idadi hii ikiwa haiakisi ukubwa wa tatizo na madhara halisi ya ajali kazini, magonjwa kwa wafanyakazi, familia na uchumi.

Shirika hilo la kazi dunianiILO linasema kwamba taarifa sahihi za kitaifa zinahitajika ili kufahamau uhalisia wa ukubwa madhara wa ajali kazini, majeruhi, magonjwa na uanzishwaji wa sera na mikakati ya usalama na afya katika maeneo ya kazi.

ILO imesema ikiwa nchi zitapata takwimu sahihi za matukio hayo, itawezesha kuchukua hatua zikiwamo utambuzi wa hatari na kujihami pamoja na sekta ambazo ni hatarishi kwa wafanyakazi