Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gonjwa lisilojulikana laibuka Liberia , 11 wapoteza maisha:WHO

Gonjwa lisilojulikana laibuka Liberia , 11 wapoteza maisha:WHO

Watu 11 wamepoteza maisha na wengine wanane bado wako hospitali na wawili katika hali mbaya nchini Liberia, baada ya kuibuka gonjwa lisilojulikana na kuwakumba watu 19 tangu Jumatatu Aprili 24. Joseph Msami na taarifa kamili

(TAARIFA YA MSAMI)

Shirika la afya ulimwenguni linasema limepokea taarifa kutola wizara ya afya ya Liberia kuhusu ugonjwa huo usiojulikana na vifo kwenye hospitali ya Francis Grant mjini  Greenville, kata ya Sinoe Kusini Mashariki mwa Monrovia.

Idadi kubwa ya waathirika ni vijana walio chini ya umri wa miaka 21. Hata hivyo WHO inasema vipimo vimeonyesha kuwa ugonjwa huo sio Ebola. Fadela Chaib ni msemaji wa WHO

(SAUTI FADELA)

"Timu za dharura zimewekwa tayari katika ngazi ya Wilaya na Kata kwa msaada wa kiufundi na vifaa kutoka WHO, CDC na wadau wengine.Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa, kutapika, maumivu ya kichwa, na kuhara.Timu za dharura zinachunguza ripoti za kuhusisha mlipuko huop na kuhudhuria mazishi ya kiongozi mmoja wa dini"