Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuchukue hatua sasa kukomboa watu wa Syria-O'Brien

Tuchukue hatua sasa kukomboa watu wa Syria-O'Brien

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetakiwa kuchukua hatua sasa, kuhusu Syria ili kunusu raia wa nchi hiyo wanaokabiliwa na madhila kila uchao kutokana na vita.

Akihutubia baraza hilo Alhamisi mjini New York Marekani, mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura (OCHA) Stephen O'Brien, amesema umoja huo unaamini hakuna suluhisho la nguvu za kijeshi dhidi ya mgogoro huo.

O'Brien amehutubia baraza la usalama kwa njia ya video kutoka mjini Geneva Uswisi wakati huu ambapo raia wa Syria wameingia mwaka wa saba wa mgogoro nchini mwao, uliogharimu maisha ya zaidi ya watu 250,000.

Amesema mashambulizi ya hivi karibuni yakiwemo yale yanayodaiwa kuwa ya kemikali yanastua jumuiya ya kimataifa na kuongeza madhila kwa raia wasio na hatia.

(Sauti O'Brien)

‘‘Kwakuwa njia za kijeshi ndiyo zitumikazo sasa badala ya suluhisho la kisiasa, hakuna amani ya kudumu. Matokea yake ni raia kuendela kuteseka. Tunahitaji hatua sasa kwakuwa tumechelewa. Kwahiyo wajumbe wa baraza la usalama, ni vitendo sasa vitakavyotoa mwelekeo’’.

Amesisitiza umuhimu wa pande kinzani kuruhusu misaada kuwafikia wahitaji