Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres amteua Edmund Mulet kuongoza jopo la uchunguzi la UM na OPCW

Guterres amteua Edmund Mulet kuongoza jopo la uchunguzi la UM na OPCW

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres leo ametangaza kuteuliwa kwa Edmund Mulet wa Guatemala kuongoza jopo huru la watu watatu watakaoongoza mfumo wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Shirika la Kupinga Silaha za Kemikali (OPCW) kuhusu matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.

Mfumo huo (JIM) uliwekwa na azimio la Baraza la Usalama 2235 (2015), na mamlaka yake yaliongezwa kwa mwaka mmoja kuanzia Novemba 17 2016, kupitia azimio 2319 (2016) la Baraza hilo.

Katibu Mkuu ametoa shukrani kwa mkuu wa JIM anayeondoka, Virginia Gamba wa Argentina, kwa kujituma, umahiri na ubobezi wake kitaaluma. Bi Gamba atachukua wadhfa mpya kama Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Watoto na Migogoro ya Silaha.

Bwana Mulet aliwahi kuhudumu kama Msimamizi Mkuu wa Umoja wa Mataifa, chini ya Katibu Mkuu wa zamani Ban Ki-moon. Kabla ya hapo, alikuwa Msaidizi wa Katibu Mkuu katika Opereseheni za Ulinzi wa Amani, kati ya 2007 na 2015.