Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya vifo na majeruhi yaongezeka Afghanistan-UNAMA

Idadi ya vifo na majeruhi yaongezeka Afghanistan-UNAMA

Mpango wa Umoja wa mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) umezitaka pande zote katika mgogoro kuchukua mara moja hatua madhubuti za kuwalinda vyema raia wasidhurike, wakati huu ambapo takwimu za mwaka 2017 zilizotolewa leo Alhamisi na UNAMA zikionyesha kuendelea kwa idadi kuwa ya raia wanaodhurika kwenye machafuko.

Kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini humo Tadamichi Yamamoto raia wengi wakiwa wanawake na watoto ndio wanaobeba gharama kubwa ya vita nchini humo.

Katika robo ya kwanza ya 2017 UNAMA imeorodhesha raia 2181 walioathirika, 715 kati yao wameuawa na 1466 kujeruhiwa ikiwa ni ongezeko la asilimi 4 ikilinganishwa na wakati kama huu 2016.

UNAMA inasema Kabul ndio iliyoshuhudia idadi kubwa ya waathirika kutokana na mashambulizi ya kujitoa muhanga , ikifuatiwa na majimbo ya Helmand, Kandahar, Nangarhar na Uruzgan.