Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha fursa nyingine ya kufikisha misaada Sudan kusini:

UM wakaribisha fursa nyingine ya kufikisha misaada Sudan kusini:

Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Marta Ruedas, leo amekaribisha uzamuzi wa serikali ya Sudan kufungua upenyo wa tatu kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kuweza kusafirishwa kutoka Sudan kwenda kwenye maeneo yanayokabiliwa na baa la njaa Sudan kusini.

Amesema upenyo huo mpya kutoka El Obeid katikati mwa Sudan kwenda mji wa Aweil jimbo la Bahr el Ghazal Sudan kusini utaruhusu shirika la mpango wa chakula duniani WFP kufikisha tani zingine 7000 za mtama ili kusaidia watu 540,000 wanaohitaji msaada wa chakula.

WFP imesema msafara wa kwanza wa msaada huo utaondoka wiki ijayo. Mamilioni ya watu wanahitaji chakula na msaada wmingine Sudan Kusini na kufikisha msaada kupitia Sudan ni rahisi zaidi amesema Bi Ruedas.

Hadi sasa tani zaidi ya 70,000 za vyakula na bidhaa nyingine vimepelekwa Sudan Kusini.