Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waatalam wa IAEA wakutana kumulika umwagikaji mafuta baharini

Waatalam wa IAEA wakutana kumulika umwagikaji mafuta baharini

Wataalam kutoka nchi 16 wanakutana wiki hii kwenye maabara ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) mjini Monaco, ili kufanyia tathmini mbinu za kisasa za kuchunguza vyanzo vya mafuta yanayomwagika baharini na kutia hatarini maisha ya viumbe wa majini.

Mkutano huo wa kila mwaka wa mtandao wa wataalam wanaofuatilia umwagikaji mafuta unafanyika kwenye maabara ya IAEA kwa mara ya kwanza, ukileta pamoja wataalam 35 kutoka taasisi za serikali, sekta binafsi na vyuo vikuu.

Wataalam hao wanajadili mbinu tofauti za kufuatilia vyanzo vya janga la kimazingira la umwagikaji mafuta baharini.

Shirika la IAEA linatoa maarifa katika mbinu za kinyuklia na kiisotopiki, ambazo husaidia nchi kutambua vyanzo vya mafuta yalomwagika baharini, na katika kupanga vyema hatua za kukabiliana na umwagikaji huo.