Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasichana washikamana kuonyesha ujuzi wao katika teknolojia-ITU

Wasichana washikamana kuonyesha ujuzi wao katika teknolojia-ITU

Siku ya kimataifa ya wasichana katika teknolojia ya mawasiliano ICT imeadhimishwa Alhamisi April 27 kote duniani kwa kuonyesha ujuzi wa teknolojia kwa wasichana na wanawake. Joseph Msami na taarifa kamili

(TAARIFA YA MSAMI)

Siku hii inatanabaisha thamani ya mwanamke katika nyanja ya habari na teknolojia ya mawasiliano na kuchagiza wasichana wengi zaidi kuwa na mipango ya kuingia katika tasnia hii ili kupanua wigo wake.

Siku hii ambayo huandaliwa kila mwaka na muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU, mwaka huu nia imekuwa kuwakutanisha wasichana kifikra Geneva, Vilnius na Beirut kupitia apu ya mchezo wa pamoja wa kuanganishwa kwa njia ya video.

Hii imewawezesha wasicha hao kutathimini ICT kwa pamoja huku wakibadilishana mawazo wakati huohuo. ITU inataka kuwawezesha wanawake na makampuni ya ICT kukumbatia faida ya kuwa na wanawake wengi katika tasnia ya ICT.