Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta rasmi yainua wanawake wajenzi Bolivia- ILO

Sekta rasmi yainua wanawake wajenzi Bolivia- ILO

Shirika la kazi duniani ILO limeripoti katika wavuti wake kuwa kundi la wanawake huru wajenzi 250 nchini Bolivia wameimarisha mazingira ya kazi zao, hatua inayowawezesha kuwa na muda na familia.

Katika makala maalum inayomulika mwanamke Lidia Romero mwenye umri wa miaka 43 ambaye ni mwanamke wa jamii ya watu asilia nchini humo, ambaye kwa miaka mitatu amekuwa akifanya kazi katika sekta ya ujenzi, anasema awali aliajiriwa katika sekta isiyo rasmi

‘‘Walinifanya nifanye kazi bila malipo, Ikiwa ningefahamu haki zangu kazini, ningeweza kutoa malalamiko yangu,’’ anasema Lidia ambaye kila asubuhi humpeleka mwanaye shuleni na kisha kukutana na wanawake wenzake kutekeleza wajibu wao."

Lidia anasema kwakuwa alifanya kazi bila malipo, sasa amemakinika, kwani anasaini mkataba kabla ya kuanza kazi ili kuepkuka kurejelea makosa. Kwa mujibu wa ILO mkataba kama huo humwezesha mwajiri kuamni kuwa yeye na wenzake watatimiza wajibu wao kwa mujibu wa makubaliano.

Shirika la kazi duniani ILO linasema kuwa usalama na afya ni muhimu kwa wanawake makazini hususani katika sekta ya ujenzi.