Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa kupinga silaha za kemikali watimiza miaka 20

Mkataba wa kupinga silaha za kemikali watimiza miaka 20

Jitihada za kupambana na silaha za kemikali ziko katika tisho kubwa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumatano. Katika salamu za pongezi kwa shirika la kupinga matumizi ya silaha za kemikali (OPCW) na mkataba kuhusu silaha hizo vikisherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa. Guterres amesema ingawa kumepigwa hatua kuna walakini.

(SAUTI GUTERRES)

“Karibu nchi zote ni wanachama wa mkataba huo, na shirika limesaidia kutokomeza kiasi kikubwa cha silaha hizo duniani, lakini hatua hizo ziko katika tisho, Mashariki ya Kati watu wanavunja mwisko dhidi ya silaha hizo na shambulio la karibuni Syria ni kumbusho la vigingi hivyo”

Ameongeza kuwa hakutokuwa na ukwepaji sheria kuhusu uhalifu wa matumizi ya silaha hizo akitumai kwamba nchi zote zitaunga mkono juhudi za OPCW na mkakati wa Umoja wa Mataifa kuhusu silaha za kemikali.