Jamii za wawindaji zilindwe-Milka

26 Aprili 2017

Kufurushwa kwa jamii za wawindaji misituni kunaathiri ustawi na kuvunja haki za binadamu kwa jamii hizo za wawindaji, amesema Milka Chepkorir kutoka jamii ya watu wa asili ya Sengwer anayefanya kazi na shirika la kimataifa la kutetea watu wanaoishi misituni.

Akizungumza na idhaa hii katika mahojiano maalum, Bi Milka anayehudhuria mkutano wa 16 wa jukwaa la kudumu kuhusu masuala ya jamii asilia, amesema wanawake,wasichana na watoto wa wawindaji hususani jamii ya Sengwer nchini Kenya hupitia madhila pindi wanapoondolewa misituni.

(Sauti Milka)

Kuhusu anachotarajia baada ya mkutano huo, binti huyo mwanaharakati amesema.

(Sauti ya Milka)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter