UM wataka uchunguzi na hatua dhidi ya mauaji ya wafanyakazi wake DRC

UM wataka uchunguzi na hatua dhidi ya mauaji ya wafanyakazi wake DRC

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Jumanne umeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kufanya uchunguzi wa kina na wa wazi dhidi ya mauaji ya wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa na watu wengine nchini humo. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Wito huo umekuja baada ya kutolewa video inayoonyesha jinsi wataalamu hao walivyouawa . Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Ravina Shamdasani wafanyakzi wa Umoja wa Mataifa DRC wameiona video hiyo na amesema wahusika wanahitaji kufikishwa mbele ya sheria kwa misingi ya viwango vya kimataifa vya haki za binadamu na ukwepaji sheria lazima ukomeshwe nchini humo.

Kuhusu hatima ya wafanyakazi wengine wawili ambao ni raia wa Congo waliotoweka pamoja na wataalamu hao, amesema hakuna taarifa zozote mpya hadi sasa.